Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama mkoani Mwanza limewakamata watuhumiwa 116 wanaodaiwa kuhusika katika uchochezi wa uwepo wa maandamano Desemba 9 2025.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mtafungwa, amesema kuwa watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa na uchunguzi ukikamilika, watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.
Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetoa wito kwa wananchi kutojihusisha au kushirikishwa katika maandamano hayo ambayo tayari yamekatazwa rasmi.
Aidha amewahimiza Wazazi na walezi kuwazuia watoto wao kujiingiza katika shughuli hizo na kushirikiana na Serikali katika kudumisha amani, utulivu na mshikamano katika siku ya kumbukizi ya Uhuru wa Tanganyika.