Michezo - Radio Kwizera

Michezo

SIMBA 1

Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pongezi kwa klabu ya Simba

Ametuma salamu hizi baada ya kufanikiwa kufuzu hatua ya Nusu Fainali katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika

Kupitia mitandao yake ya kijamii ameandika “Pongezi za dhati kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup). Ushindi wenu ni furaha kwa mashabiki wenu na burudani kwa Watanzania wote. Ninawatakia kila la kheri katika Nusu Fainali.” Rais Samia ameandika.

Simba imetinga hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) kufuatia ushindi wa penalti 4-1 dhidi ya Al Masry ya Misri kwenye robo fainali.

FT: Simba Sc  2-0 Al Masry Agg. 2-2
⚽ 22’ Mpanzu
⚽ 32’ Mukwala

MATUTA:
🇹🇿 Simba Sc: ✅✅✅✅

🇪🇬 Al Masry: ❌ ✅❌