
Vikosi vya chama cha upinzani cha SPLM/A-IO vya nchini Sudan Kusini vimekataa amri iliyotolewa na Jeshi la Ulinzi la nchi hiyo, kutaka askari wake wakusanyike katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali.
Msemaji wa jeshi la upinzani Lam Paul Gabriel amesema, vikosi hivyo ni huru na vinapokea amri kutoka kwa uongozi wake pekee, na sio Jeshi la Sudan Kusini.
Hatua hiyo imekuja baada ya amri kutoka kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Sudan Kusini, kuwataka askari wa SPLM/A-IO ambao wamejificha kufuatia mapigano kati ya pande hizo mbili karibu na mji mkuu wa Juba, kuripoti katika kambi za jeshi hilo ama vituo vyake vilivyo nje ya kambi.