Habari - Radio Kwizera

Habari

Mwanza

Mahakama ya wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza imemhukumu miaka 60 gerezani mkazi wa kijiji cha Kinamweli kwa kosa la kubaka na kumsababishia ujauzito mwanafunzi mwenye umri wa miaka 14

 

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Ndeko Dastan Ndeko ambapo amesema mshatakiwa Iddy Renatus Makungu mwenye umri wa miaka 30 alitenda kosa kwa nyakati tofauti kati ya mwezi wa 4 na 5/ 2024 kijijini hapo wilaya humo

Kwa mujibu wa Hakimu Ndeko, mshtakiwa alitenda kosa hilo katika kesi ya jinai namba 31962 ya mwaka 2024 kinyume na vifungu vya 130(1)(2)(e) na 131(1) vya Kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022

Mwendesha mashtaka wa Serikali Juma Kiparo amesema kuwa Mshtakiwa alifikishwa kwa mara ya kwanza Mahakamani hapo tarehe 11,11,2024 na kusomewa mashtaka ya kubaka na kumpa mimba binti huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne na mshtakiwa kukana kutenda makosa hayo yote mawili

Hata hivyo, Mahakama ilitupilia mbali utetezi huo kwa kukosa mashiko na kumhukumu mshtakiwa kwenda jela miaka 30 kwa kila kosa na kuelekeza kwamba adhabu hizo zitakwenda pamoja, hivyo mtuhumiwa atatumikia miaka 30