Serikali ya Benin imetangaza kuwa imefanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi lililofanywa na baadhi ya wanajeshi wa taifa hilo la Afrika Magharibi.
Mapema leo, kundi la wanajeshi lilitoa matangazo kwenye runinga yakidai kwamba yamepindua na kumvua madaraka Rais Patrice Talon.
Mshauri wa rais ameeleza kuwa kiongozi huyo yuko salama na yuko katika ubalozi wa Ufaransa.
Mapema asubuhi kundi la wanajeshi wametangaza kupitia televeisheni kuwa wamechukua madaraka na kumuondoa Rais Patrice Talon na muda mfupi wanajeshi watiifu serikalini wamezuia jaribio hilo.
Benin, koloni la zamani la Ufaransa, kwa muda mrefu imejulikana kama moja yanchi zenye demokrasia thabiti na wazalishaji wakubwa wa pamba barani Afrika ingawa inasalia miongoni mwa nchi masikini zaidi duniani.