
Na, Jerome Robert
JERUSALEM
Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas imesema Shambulizi la anga la Israel limeharibu sehemu ya hospitali katika mji wa Gaza.
Video iliyowekwa mtandaoni ilionekana kuonyesha moto mkubwa na moshi ukifuka kutoka Hospitali ya Al-Ahli Baptist baada ya makombora kugonga jengo la ghorofa mbili.
Watu, pamoja na baadhi ya wagonjwa ambao bado wako kwenye vitanda vya hospitali, walirekodiwa wakikimbia kutoka kwenye eneo hilo.
Hamas ilitaja shambulio hilo kuwa uhalifu wa kutisha wa Israel, ambayo ilisema inachunguza ripoti hizo, japo limesema kuwa hakuna majeruhi walioripotiwa, kulingana na huduma ya dharura ya kiraia.