Rapper wa Tanzania anayeishi Munich, Ujerumani, @para_chich ameachia album yake yenye nyimbo 14 iitwayo Sell Out.
Para Chichi amesema kuwa Sell Out imebeba ujumbe mzito unaangazia tabia ya watu kujitoa thamani yao ya ndani kwa faida ya nje.
Pia ameongezea kuwa album hii inazungumzia maumivu, mapenzi, majaribu, ego na nidhamu kwa sababu katika kila moja ya nyakati hizo unakuwa na uchaguzi Kubaki imara au kuuza vipande vya nafsi yako kwa ajili ya faraja.
Kwenye Sell Out kuna wimbo mmoja pekee aliowashirikisha wasanii wengine, Fight ambao amewashirikisha Rapcha na Marleen Xplastaz.
