Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Iimewakamata watuhumiwa 12 wa uhalifu, wakiwa wamejificha kwenye mapango Mkoani humo, wakidaiwa kuwa na vifurushi vya bangi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, amesema operesheni hiyo ilianza rasmi Novemba 29, 2025, ikihusisha maeneo ya Kata za Mkolani, Buhongwa, Isamilo.
Nyingine ni Mhandu, Igoma Kati na Mahina Wilaya ya Nyamagana na Kitangili, Bwiru Ziwani, Kawekamo na Ibungilo, Wilaya ya Ilemela.
Kamanda Mutafungwa amesema Jeshi la Polisi litaendelea na operesheni maalumu katika maeneo ya milima na mapango yanayotajwa kuwa maficho ya wahalifu, kutokomeza uhalifu Mkoani humo.