Rais wa CAF, Patrice Motsepe, amesema mwimbaji Burna Boy alizuiliwa kwa muda katika uwanja wa ndege nchini Morocco baada ya maafisa wa forodha kuhoji vito vingi vya dhahabu alivyokuwa navyo.
Tukio hilo liliwalazimu viongozi wa CAF kumwasiliana na Motsepe, ambaye aliingilia kati na kulitatua, na hivyo Burna Boy akaendelea na safari yake hadi Rabat kwa ajili ya burudani ya AFCON Fan Zone.
Burna Boy mara nyingi huwasilisha ujumbe unaohusu maisha ya Mwafrika, mapambano ya kijamii na kisiasa, pamoja na kujivunia utamaduni wa Afrika. Hii ndiyo sababu amekuwa sauti muhimu inayowakilisha Afrika katika muziki wa kimataifa.