
Na, Elias Zephania
CHATO
Umoja wawamiliki wa vyuo vya afya nchini umeahidi kuwasomesha fani ya udaktari wasichana wanne mapacha wanaosoma kidato cha tatu shule ya sekondari Zakia Megji baada ya kutelekezwa na wazazi wao.
Mwenyekiti wa umoja huo, Dkt Joel Maduhu amesema kuwa ameguswa na changamoto wanazopitia mabinti hao katika masomo na kuahidi kuwasomesha udaktari pindi watakapo hitimu masomo yao ya sekondari.
Amesema kitendo cha mapacha hao kutelekezwa na wazazi wao hakina afya katika harakati za kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na kwamba jamii nzima ina kila sababu ya kushirikiana katika kutimiza ndoto za watoto hao.
Mapacha hao wameushukuru umoja huo kwa kuwatembelea na kuwatia moyo na kuahidi kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao pamoja na kutoa wito kwa jamii na wasamaria wema kuendelea kujitokeza kutatua changamoto zinazowakabili.