
Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama mkoani Shinyanga inampango wa kuzifikisha mahakamani kampuni 34 zinazofanya kazi mgodi wa BARRICK Bulyanhulu Wilayani humo kwa kutolipa kodi ya huduma kwa serikali
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga na mkuu wa wilaya ya Kahama Bi Mboni Mhita katika Baraza maalumu la madiwani la Halmashauri hiyo kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali (CAG)
Bi Mhita amesema hawana budi kama Serikali kuchukua hatua za kisheria kwa kampuni hizo kwasababu mazungumzo ya mwanzo yameshindwa kuzaa matunda.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ibrahim Six Diwani wa kata ya Mwakata amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuchukua hatua za kisheria mara moja ili kuokoa mapato yanayoendelea kupotea.
Aidha Redio Kwizera inaendelea na jitihada za kuutafta uongozi wa mgodi huo kufahamu chanzo kinachosababisha makapuni hayo kutolipa mapato kwa serikali.