
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi CCM, Ally Hapi amesema ripoti ya CAG sio hukumu ya Mahakama kwamba wanaotajwa wote moja kwa moja huwa ni Mafisadi au Wezi bali ripoti husomwa kisha kuwapa nafasi Watumishi na Taasisi kutoa vielelezo ambavyo havikuwasilishwa wakati wa ukaguzi.
Akiongea Jana katika mdahalo Ally Hapi amesema taarifa ya CAG Watu wengi wakisikia inasoma wanadhani ni hukumu ya Mahakama
Aidha amesema CAG ikishakamilisha ukaguzi huhitaji listi na vielelezo na kama kunabainika hoja taasisi zinatakiwa kuzijibu