
Wakazi wa Kata ya Nyakabango Wilayani Muleba Mkoani Kagera wameshauri uongozi wa kambi ya wavuvi wa mwaro wa Magarini kudhibiti wavuvi wanaotoka Wilaya jirani kutega samaki kwa kutumia nyavu haramu kisheria
Bw Emmanuel marauli na Dellphina Deliphinius wamesema kuwa katia hiyo imekuwa na changamoto ya baadhi ya wavuvi kutoka nje ya Wilaya hutenga samaki kwa nyavu haramu majira ya usiku.
Wamesema hali hiyo inaathiri mazalia ya samaki kwasababu wavuvi wa Kata hiyo wamekuwa wakifuata sheria na kuuomba uongozi wa kambi hiyo kudhibiti wavuvi hao na tayari wamejiswekea sheria zao.
Mwenyekiti wa Mwaro wa Magarini Bw. Radislaus Pamba amesema wamekuwa wakifanya doria kukabiliana na changamoto hiyo licha ya kukosa taarifa za uhakika kuhusu watu hao ili sheria ichukue mkondo wake.