
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa’ichi amekemea watu wanaokimbilia kwa waganga wa kienyeji na sehemu zisizofaa kutafuta ufumbuzi wa changamoto badala ya kumtegemea Mungu.
Amesema hayo wakati wa misa takatifu ya kuwapandisha daraja la upadri mashemasi 11 katika kituo cha Msimbazi Dar es Salaam jana.
amesema naweza kukuta mtu anaenda kwa waganga wote kutafuta ufumbuzi au anaenda kwa wakorofi na walaghai kutafuta jibu, lakini huko ni kurubuniwa mara nyingi kwani anayetoa uzao ni Mungu si binadamu.
Mapadri hao ni Fransisco Benedicto, George Mbago, Benjamini Maganga, Josephat Mlacha, Gabriel Kiondo, na Mark Clement.
Wengine ni Richard Hazvado, Emmanuel Lazaro, Christian Leonard, Charles Msabila na Kanuth Martin.
Ruwa’ichi aliwataka mapadri hao wasimame imara katika kufanya kazi takatifu ya Mungu bila kulalamika.