
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakitapokea mchango wowote unaoweza kudhalilisha heshima na uhuru wa Tanzania katika harambee yake inayotarajiwa kufanyika kesho jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi, akizungumza leo Jumatatu, Agosti 11, 2025, amesema kuwa michango yote itakayopokelewa itachunguzwa chanzo chake kabla ya kukubaliwa.
CCM inalenga kukusanya Sh100 bilioni kupitia harambee hiyo, huku ikieleza fedha hizo zitatumika katika maandalizi ya kampeni za uchaguzi mkuu.
Dk Nchimbi amesema kwa sasa CCM ina wanachama 13.19 milioni waliowasajili kupitia mfumo wa mtandao.