
Na Shafiru Yusuph- Muleba, Kagera
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoa wa Kagera imefanya maadhimisho ya juma la Watu Wazima kimkoa ambayo imeambatana na maonesho wadau hao ndani na nje ya mfumo rasmi wa elimu ambayo yamefanyika Wilaya ya Muleba.
Mkufunzi Mkazi wa Mkoa wa Kagera kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Bw. Charles Mkwidu amesema hadi sasa jumla ya mabinti 264 waliokatizwa na masomo ya sekondari kwa sababu mbalimbali zikiwemo ujauzito wamerudishwa shuleni mkoa wa Kagera kwa kipindi cha miaka minne.
Wanafunzi hao wameendelewa kusomeshwa bila malipo na Serikali kupitia mpango wa kuboresha elimu ya Sekondari kwa njia mbadala (SEQUIP-AEP).
Mkwidu amesema kuwa kwa mwaka 2022 waliosomeshwa bure ni mabinti 92, mwaka 2023 walikuwa 57, mwaka 2023 walikuwa 43 na mwaka huu wa 2025 walikuwa 72.
Naye Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Kagera Bw. Simon Chiboni amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuhamasisha jamii ili kutambua fulsa za elimu za watu wazima kupitia Wadau na kutambua mchango wa wadau kupitia taasisi mbalimbali ikiwemo changamoto pamoja na mafanikio.