
Mwenyekiti wa bodi ya Uwekezaji ya UTT AMIS Profesa Faustine Kamuzora amewashauri vijana ambao ni kundi kubwa na wenye nguvu ya kufanyakazi Kuwekeza katika shughuli mbali mbali ili wapate mtaji wa kujinyanyua kiuchumi katika maisha yao
Profesa Kamuzora amesema hayo leo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kwenye Kufungua kituo cha uwekezaji UTT AMIS huku akieleza kuwa lengo la Kituo hicho ni kuwawezesha wananchi kuondokana na wimbi la umasikini huku ikiendeleza dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 hadi 2050.
Mkurugenzi Mtendaji wa Uwekezaji UTT AMIS Simon Migangala amesema ameishukuru serikali kwa kuwawekea mazingira mazuri ya uwekezaji na kuwa bora katika kuhudumia wananchi na kuhakikisha wanawekeza na kupata faida kwa uwekezaji wao kama taasisi inayomilikiwa na serikali
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga Frank Nkinda amesema tathimni iliyofanyika na kufungua kituo hiki imethihirisha kupanua wigo na kuwawezesha wananchi kupata elimu ya fedha na kuweka akiba itakayochochea na kuleta hamasa kwa wananchi wa mjini na vijijini katika uwekezaji wao
Baadhi ya wananchi walio hudhuria ufunguzi huo Herieth John na Daud James wamesema uwekezaji huo ni mzuri utawafanya kuinuka zaidi katika biashara zao na kusomesha watoto