
Mkazi wa kijiji cha Musenyi kata ya Bisibo wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera Faida Rudendeli miaka 20 amekutwa amejinyonga kwenye mti kwa kutumia kipande cha chandarua nje kidogo ya nyumbani kwake.
Mwenyekiti wa kijiji cha Musenyi Bw. Felecian Rugage, ameiambia Radio Kwizera kuwa tukio hilo limetokea usiku wa August 20 majira ya saa 3:30 na marehemu alikuwa mkazi wa kitongoji cha Marumba.
Bw. Rugage amesema chanzo cha tukio hilo, kinadaiwa ni mgogoro wa kifamilia ambapo marehemu alikuwa na ugomvi na mke wake.
Jeshi la polisi limefika kijiji cha Musenyi wakiwa na daktari na baada uchunguzi wameruhusu mwili wa marehemu kuzikwa wakati upelelezi ukiendelea.