
Msanii wa muziki kutoka Nigeria Tiwa Savage ameeleza kufurahishwa na namna Diamond anavyofaya kazi na ni shabiki wa muziki wake.
Ameendelea kwa kusema Diamond ndio kauweka muziki wa Bongo Fleva kwenye ramani ya muziki duniani.
Diamond anatambulika kama mmoja wa wasanii wakubwa Afrika, akipata tuzo nyingi, kufanya shoo ndani na nje ya Afrika, na kushirikiana na mastaa wakubwa duniani.
Ameongea hayo kwenye mahojiano yake kwenye kipindi cha The Breakifast Show kutoka Marekani.
Miongoni mwa nyimbo ambazo zilizomtambulisha Tiwa Savage ni “Kele Kele Love”, “Eminado”, “All Over”, na “Somebody’s Son” aliyomshirikisha Brandy.
Pia amepata tuzo nyingi ikiwemo MTV Africa Music Awards, Headies, na pia kuwa mwanamuziki wa kwanza wa kike kutoka Afrika kusaini mkataba na Universal Music Group mwaka 2019.