
Miss Tanzania 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi, amemuandikia barua ya wazi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiweka bayana changamoto zinazokumba watoto waliopoteza mzazi, hasa baba.
Katika barua yake, Jacqueline Mengi anasema kuwa haki za watoto kupata malezi na urithi mara nyingi hazitekelezwi, na hivyo kuacha mama mchanga aliyeachiwa mali na huzuni akipitia mateso mapya kutokana na udhaifu wa mifumo ya usimamizi wa mali.
Jacqueline Mengi anabainisha kuwa dhuluma hii inawaathiri zaidi watoto wanaopoteza baba, ambao wanakosa usalama na ulinzi wakati wanapohitaji uthabiti.
Na hivyo anamuomba Rais Samia kuhakikisha kuwa wasimamizi wa mali za marehemu wanawajibishwa kikamilifu, huku kuwepo na ukaguzi mkali dhidi ya matumizi mabaya ya mamlaka.
Na mama aliyeachwa wakiwa bado vijana na watoto wao wapate ulinzi maalumu ili wasibaki bila msaada kutokana na mianya ya mifumo ya udhaifu.
Jacqueline amehitimisha kwa kuomba kuwa viongozi wa taifa wawe mstari wa mbele kulinda haki za watoto, na hivyo kuhakikisha kuwa hakuna mtoto anayepitia dhuluma.