
Polisi wameeleza kuwa Celeste Rivas (15), ambaye mwili wake ulipatikana hivi karibuni kwenye gari la msanii chipukizi D4vd, alifanikiwa kuishi kwa muda mrefu bila kugundulika kwa kutumia vitambulisho bandia vilivyomfanya aonekane kama mtu mzima.
Kwa mujibu wa taarifa za TMZ, wachunguzi wanaamini kuwa kuna ushahidi mwingi unaoonyesha Celeste alitokea kwenye mazingira magumu ya kifamilia, jambo linalodaiwa kuchochea uamuzi wake wa kutoroka nyumbani.
Mmiliki wa duka la pombe karibu na kituo cha basi cha shule ya Celeste alisimulia tukio la Machi 19, 2024, ambapo dada yake Celeste alifika dukani hapo akiomba kuangalia kamera za usalama kwa matumaini ya kufuatilia nyayo za dada yake aliyekuwa amekimbia.
Taarifa hizi mpya zinaongeza maswali zaidi kuhusu maisha ya Celeste, mazingira yaliyomzunguka, na ni kwa namna gani aliweza kuishi muda mrefu bila kurejea nyumbani – hadi mwili wake ulipopatikana kwenye Tesla iliyosajiliwa kwa jina la msanii D4vd (David Anthony Burke)