
Mwanamitindo mtanzania anayeishi nchini Ufaransa, @miriamodemba, amesema lengo la kuanzisha jukwaa la mitindo la Sauti ya Mitindo ni kuwapa fursa vijana, bara na visiwani kutimiza ndoto zao.
Hatua hiyo imekuja baada ya mlimbwende aliyeshika nafasi ya pili Miss Mtwara University Bonanza kuomba kukutana na Miriam amsaidie kutimiza ndoto zake.
Akijibu ombi hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Miriam amesema nakuombea kheri kwenye ndoto zako, na ukafanikiwe zaidi natumaini tutaonana, nitafurahi kukuona pia nikiwa mjini.