
Mariah Carey amefafanua kilichotokea baada ya video yake kusambaa ikitafsri kutoridhishwa wakati Muni Long akiimba wimbo “We Belong Together” kwenye tuzo za iHeartRadio Music Awards 2025.
Akizungumza kwenye mahojiano mapya, Carey amesema hakujua kabisa kwamba Muni Long angefanya heshima hiyo na hakusikia vizuri uimbaji huo kutokana na tatizo la sauti ukumbinina ameeleza kuwa kwa kawaida hapendi watu kuimba nyimbo zake, akifananisha mtazamo wake na ule wa Prince, ingawa alisisitiza kuwa alihisi kuheshimiwa na kuguswa na tukio hilo.
Kwa upande wake, Muni Long tayari alikuwa amebainisha kuwa Mariah Carey mwenyewe alimwomba aimbe wimbo huo kama heshimna aidha, Muni Long alisema ana ushahidi wa video ukimuonyesha Carey akimsifia nyuma ya jukwaa lakini hakutaka kuuchapisha.
Kwa ufupi, Carey ameeleza kuwa uso wake uliokunjika haukuwa ishara ya kutomkubali Muni Long, bali zaidi ni mshangao na hali yake ya kutopenda nyimbo zake kuimbwa na wengine.