
Mtayarishaji na mfanyabiashara maarufu wa muziki nchini Nigeria, Don Jazzy, amefichua gharama zinazohitajika ili kumtambulisha msanii mpya chini ya lebo yake ya Mavin Records.
Akizungumza kupitia Echo Podcast, mwanzilishi huyo wa Mavin amesema kuwa kumutengeneza rasmi msanii hadi kumtambulisha kunagharimu kati ya dola 100,000 hadi 300,000 (takribani milioni 200 mpaka 600 za Kitanzania).
Don Jazzy amebainisha kuwa kiwango hicho kinahusisha mchakato mzima wa kumtengeneza staa mpya kuanzia muziki, video, promosheni, hadi kujenga jina la msanii kwenye soko la kimataifa.
Kwa miaka mingi, Mavin Records imezalisha mastaa wakubwa kama Rema, Ayra Starr, Ladipoe, na Crayon, ikidhihirisha uwekezaji mkubwa unaowekwa nyuma ya mafanikio yao