
Cardi B ameshika nafasi ya kwanza kwa mara ya pili kwenye chati ya Billboard 200 baada ya albamu yake mpya AM I THE DRAMA? kuingia rasmi ikiongoza chati ya Oktoba 4, ikiwa imeuza units 200,000 (equivalent album units) nchini Marekani kwa wiki iliyoishia Septemba 25, kwa mujibu wa takwimu za Luminate.
AM I THE DRAMA? ni albamu ya pili ya Cardi B, ikitoka miaka saba baada ya albamu yake ya kwanza Invasion of Privacy (2018) iliyoshinda tuzo ya Grammy na pia kuongoza chati za Billboard.
Kupitia Instagram, Cardi B amewashukuru mashabiki wake kwa kuipokea albamu hiyo kwa kishindo.
Cardi B ameandika “Asanteni sana wote mlionisaidia!! Wiki mbili zilizopita albamu ilitarajiwa kufanya 115k kwa nyimbo Outside na Imaginary Players. Sikujua itapokelewa vipi… lakini tumepita matarajio yote, Asante kwa kila mtu aliyeisikiliza, kurekodi video akicheza wimbo wangu na kila kitu! Hamjui ujasiri na nguvu mlizonipa kuendelea kusonga mbele. Siwezi kusubiri kuonana nanyi kwenye ziara. Leo tunasherehekea!!! Siwezi kufungua champagne… lakini labda nitafungua juisi ya cranberry!”
Hii ndiyo wiki kubwa zaidi ya mauzo ya 2025 kwa albamu ya msanii wa kike wa R&B/Hip-hop.