
Zuchu, amefanikisha jambo la kipekee baada ya wimbo wake mpya ‘Amanda Remix’ kufikia nafasi ya 12 kwenye vchati ya iTunes nchini Grenada, kisiwa kilicho kwenye Bahari ya Karibiani, kando ya visiwa vya Windward, karibu na Trinidad na bara la Amerika Kusini.
Mafanikio haya bila shaka yanachangiwa na ushirikiano wake na Spice, msanii mwenye mahadhi ya Caribbean, jambo lililoongeza mvuto wa wimbo huu kwa mashabiki wa nje ya Afrika.
Zuchu amesherehekea mafanikio hayo kwenye instagram akiandika ‘#AMANDA’ remix imefanikiwa kufikia nafasi kwenye iTunes Chart ya 🇬🇩 Grenada.“No.12, baby! Yess
Hii ni ishara nyingine ya ukuaji wa muziki wa Zuchu na jinsi anavyopata mashabiki nje ya Tanzania. Hongera