
Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, @aytanzania, ameandika ukurasa mpya kwenye historia ya muziki wa Tanzania baada ya nyimbo zake mbili kuzingatiwa kwenye mchakato wa kupata tuzo za Grammy mwaka 2026.
Miongoni mwa nyimbo hizo ni “Simuoni” aliyomshirikisha Harmonize, wimbo uliotolewa Mei 30 mwaka huu na kupata mapokezi makubwa ndani na ya Tanzania.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize alionekana mwenye furaha kubwa na kuandika “Inaweza isiwe leo au kesho, lakini tupo karibu! Tuendelee kusukuma! Punguza majivuno, punguza maneno, ongeza muziki, ongeza upendo! Nakipenda sana kipindi hiki!”
Hatua hii inaonesha wazi jinsi muziki wa Bongo Fleva unavyozidi kupata nafasi ya kimataifa na kusikika kwenye majukwaa makubwa duniani. Endapo AY Masta ataingia rasmi kwenye orodha ya walioteuliwa, itakuwa ni ushindi mkubwa kwa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.