
Viongozi wa dini mkoani Geita wamekumbushwa kuendelea kusisitiza hali ya uadilifu katika jamii kwa kukemea vitendo vya rushwa vinavyoweza kupoteza haki na kuzalisha dhuruma
Naibu mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Geita Alex Mpemba amesema hayo kwenye viunga vya ofisi ya TAKUKURU katika kikaokazi cha TAKUKURU na kamati ya amani ya mkoa wa Geita inayoundwa na viongozi wa dini ikiwa ni kukumbushana wajibu katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi huu wa oktoba
Mpemba amesema maadili hayawezi kuwepo kama watu watakuwa na tabia za vitendo vya rushwa ambavyo hata vitabu va dini vinakataza
Askofu Stephano Saguda ambaye ni mwenyekiti mwenza wa kamati ya amani ya mkoa wa Geita pamoja na Shehe Ibnubazi Rajabu aliyemwakilisha Shehe wa mkoa wa Geita ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo,wamesema moja ya madhara ya rushwa ni Tifa kuwa na laana
Wamesema TAKUKURU ambao wamepewa dhamana ya kuzuia, kupambana pamoja na kutoa elimu ya vitendo vya rushwa, hawana budi kuendelea kutoa elimu kila mara ili Taifa lijengwe katika misingi ya maadili
Hata hivyo baadhi ya washiriki wameomba elimu hii iwe endelevu kupitia mikutano ya hadhara, makongamano na kwenye nyumba za ibada kwa kuamini kuwa viongozi wa dini wana idadi kubwa ya watu nyuma yao ambao wakielemika, jamii itakuwa imeelimika na kuacha vitendo vya rushwa