
Msanii wa Bongo Fleva, @Rayvanny (Chui) ameandika historia mpya baada ya wimbo wake “Oh Mama! Tetema” alioshirikiana na Nora Fatehi, Vishal Mishra na Shreya Ghoshal kutumika kwenye zaidi ya reels milioni 1 kwenye Instagram.
Hii ina maana kuwa watu zaidi ya milioni moja duniani wamechagua kutumia sound ya Oh Mama! Tetema kwenye video zao, jambo ambalo mara nyingi hutokea kwa nyimbo kubwa tu za kimataifa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny alieleza kuwa huu ni ushindi wa muziki wa Tanzania na fursa ya kuonyesha kwamba Bongo Fleva inaweza kushindana kimataifa
Kwa ufikiaji huu, Rayvanny ameonyesha jinsi muziki wa Tanzania unavyoweza kupaa sio tu kwenye majukwaa ya kusikiliza muziki bali pia kwenye mitandao ya kijamii, ambapo challenge huamua ukubwa wa wimbo duniani.