
Muigizaji Francia Raisa, aliyewahi kumtolea figo rafiki yake Selena Gomez mwaka 2017 wakati wa ugonjwa wa lupus, amevunja ukimya kuhusu madai ya kutokualikwa kwenye harusi ya Selena na Benny Blanco.
Francia amesema hajawahi kuthibitisha au kukanusha kama kweli alialikwa, akisisitiza kuwa watu wamekuwa wakitengeneza tetesi nyingi zisizo na msingi.
Kauli hiyo imekuja baada ya mashabiki kudai kuwa Selena amemsahau, hasa baada ya kumuita Taylor Swift rafiki yake wa pekee katika tasnia ya burudani, jambo lililozua hisia kali mitandaoni.
Licha ya tofauti zilizodaiwa kuwepo, Francia amesema uhusiano wao haujavunjika kabisa, bali umebadilika kadri muda ulivyopita.
Wawili hao hawajazungumzia hadharani kama bado wanawasiliana, lakini mashabiki wanaendelea kutumaini marafiki hao wa watarejea katika ukaribu wao wa zamani.