
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imesema itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Wafanyabiashara wilayani kahama mkoani Shinyanga ili kufanya biashara zao ziendelee na kuchochea ukusanyaji na ulipaji wa mapato ya serikali kwa hiari.
Ahadi hiyo imetolwa October 09, 2025 na kamishina mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuf Mwenda wakati akizungumza na wafanyabiashara katika ukumbi wa mikutano wa manispaa ya kahama, ambapo amesema kuwa jukumu la TRA ni kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na kuwajengea uwezo wa kulipa kodi kwa hiari.
Kamishina Mkuu wa TRA amewatembelea wafanyabishara wadogo, wa kati, wakubwa yakiwemo makampuni ya uchimbaji madini, pamoja na kulitembelea soko la madini Kahama ikiwa ni moja ya ziara zake katia wiki ya huduma kwa wateja
Awali mfanyabiashara Faraja Shafi wa Ruchulunzi limited ameshauri na kuomba mifumo ya mamlaka hiyo kuwapa uwezo wa kupata taarifa zote wanazohitaji kama wafanyabiashara pasi kufika ofisi za mamlaka hiyo.