
Mrembo anayejulikana kama RoseyDeChocolate, ametangaza wazi kwamba ameitwa na Kituo cha Polisi kufuatia kosa la kumpiga picha msanii Harmonize akiwa amelala na kisha kusambaza picha hizo mitandaoni bila ridhaa yake.
RoseyDeChocolate amesema mbele ya polisi amekiri makosa yake na ameomba radhi na kwamba yupo tayari kuomba radhi kwa moja kwa moja kwa mhusika.
Amesema kitendo chake kilikuwa cha udhalilishaji na kisheria si sahihi, na pia si kitendo cha heshima kwa binadamu.