
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) imesema imejipanga kuendelea kujenga majengo ya ofisi kwenye mikoa na wilaya ili kuongeza utoaji wa huduma bora kwa wananchi
Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila ameeleza hayo katika uzinduzi wa jengo la TAKUKURU la wilaya ya Nyang’whale mkoani Geita ambalo limegharimu zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 386 hadi kukamilika kwake
Chalamila amesema kwa nchi nzima TAKUKURU ina ofisi 145 katika mikoa ya ki TAKUKURU 28 , wilaya 111na vituo maalumu 6 na kwamba majengo ya mikoa yanayomilikiwa na TAKUKURU ni 70 pekee ambayo ni mikoa 23, wilaya 46 na kituo kimoja
Amesema katika mwaka wa fedha wa 2025/26 TAKUKURU imepanga kujenga majengo11 ambayo yanajumuisha ofisi 1 ya mkoa, ofisi 10 za wilaya huku akieleza kuwa jumla ya ofisi 64 ambazo hazijafikiwa na kujengewa ofisi ni mikoa 4 wilaya 55 na vituo maalumu vitano na Nyang’whale ni moja ya wilaya ambazo zimeweza kufikiwa mapema katika ujenzi wa ofisi hizo
Mkurugenzi wa miliki TAKUKURU Mhandisi Dkt. Emmanuel Kiabo amesema ujenzi wa jengo la TAKUKURU wilaya ya Nyang’whale ulianza Februari 17 na kukamilika Agosti 17, 2025 kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2024,2025 chini ya utekelezaji wa force account
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Geita James Ruge amesema matarajio ya TAKUKURU ni kuongeza wadau katika kupambana na rushwa na kuongeza ali ya uwajibikaji
Chifu wa wilaya ya Nyang’whale Chief Mashauri Nzera Msalala ameipongeza TAKUKURU kwa kukamilisha ujenzi wa ofisi hiyo na kwamba utasaidia jitihada ambazo TAKUKURU wanazifanya za kuhakikisha jamii inakuwa na uelelewa juu ya vitendo vya rushwa na hatua za kuchukua