Taasisi ya Saratani Ocean Road, imesema kuna ongezeko la saratani ya matiti kwa wanaume kutoka mmoja kati ya wagonjwa wa aina hiyo ya saratani 100 mwaka 2020, kufikia watano kati ya 100 mwaka 2025.
Meneja Huduma za Uchunguzi wa Saratani na Elimu kwa Umma, Dk Maghuwa Stephano amesema saratani ya matiti imeendelea kuwa changamoto kubwa duniani huku Tanzania ikishika nafasi ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa saratani hiyo.
Saratani ya matiti kwa wanaume imeendelea kuongezeka nchini, tofauti na miaka ya nyuma ambapo idadi ya wanaume waliokuwa wakibainika kuwa na ugonjwa huo ilikuwa ndogo ikilinganishwa na wanawake.
Dk. Stephano amesema saratani ya matiti inampata mwanaume pia,tofauti na mitazamo kwenye jamii ya kuo ni ugonjwa unaowapata wanawake , hivyo kwa sasa kundi hilo wanahitajika wajikinge na kufanya uchunguzi wa mara kwa mara ili kujikinga mapema.