Natasha Stambuli, Mwanzilishi wa @igloo_ent na aliyekuwa Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania na mshindi wa tuzo ya “CEO of the Year 2021,” ametangazwa rasmi kuwa Mshauri wa GRAMMY U,
Hii ni programu ya mafunzo na ushauri kwa wanamuziki wachanga, inayosimamiwa na Recording Academy kwa kushirikiana na Amazon Music.
Kwa miaka mingi, Natasha amekuwa mstari wa mbele katika kukuza muziki na utamaduni wa Afrika katika majukwaa ya kimataifa. Uteuzi huu ni uthibitisho wa mchango wake mkubwa na dhamira ya kuendelea kuhamasisha kizazi kijacho cha wabunifu wa muziki.
Kupitia nafasi hii, Natasha atatumia uzoefu wake kuwaongoza na kuwainua vijana wenye ndoto za kufanikiwa katika sekta ya muziki duniani.