Wabunge Ridhiwani Kikwete na Wanu Hafidh Ameir ni miongoni mwa majina mapya ya Baraza Jipya la Mawaziri lenye wizara 27 lililotajwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Novemba 17, 2025 Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Kikwete – mtoto wa Rais wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete, ameteuliwa Waziri wa Ofisi ya Rais — Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora huku Wanu Ameir, ambaye ni mtoto wa Rais wa sasa, akitajwa naibu waziri wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia. Miongoni mwa mawaziri wakongwe walioachwa ni Dotto Mashaka Biteko aliyekuwa Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati ambaye wizara yake imechukuliwa na Deogratius Ndejembi.
Daniel Chongolo amechukua nafasi ya Hussein Bashe aliyekuwa waziri wa kilimo na Umwagiliaji.
Dkt Seleman Jafo aliyekuwa waziri wa Viwanda na Biashara nafasi yake imechukuliwa na Judith Slavio Kapinga, Dkt Damas Ndumbalo aliyekuwa waziri wa Katiba na sheria nafasi yake imechukuliwa na Juma Zuberi Homera.
Wengine ni Jenista Muhagama aliyekuwa waziri wa Afya nafasi yake imechukuliwa na Mohamed Omary Mchengerwa na Innocent Bashungwa aliyekuwa waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi na nafasi yake imechukuliwa na George Boniface Simba Chawene.
Wizara Muhimu ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI imechukuliwa na Prof. Liziki Silas Shemudoe.
Wizara ya Mipango na uwekezaji imebaki chini ya Prof. Alexandar Kitila Mkumbo Wakati Wizara Mpya ya Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana imeshikwa na Joel Nanauka.
Baraza Jipya la Mawaziri
Ofisi ya Rais — Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Waziri: Ridhiwani Jakaya Kikwete
Naibu Waziri: Regina Ndege Qwaray
Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji
Waziri: Prof. Kitila Alexander Mkumbo
Naibu waziri: Pius Stephen Chaya
Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana
Waziri : Joel Arthur Nanauka
Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira
Waziri: Mhandisi Hamad Yusuf Masauni
Naibu waziri: Dkt. Festo John Dugange
Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu
Waziri: William Vangimembe Lukuvi
Naibu Waziri: Ummy Hamisi Nderiananga
Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano
Waziri: Deus Clement Sangu
Naibu waziri: Rahma Riadh Kisuo
Ofisi ya Waziri Mkuu — Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Waziri: Prof. Riziki Silas Shemdoe
Naibu waziri (Elimu): Reuben Nhamanilo Kwagilwa
Naibu waziri (Afya): Dkt. Jafar Rajab Seif
Wizara ya Fedha
Waziri : Balozi Khamis Mussa Omar
Naibu waziri: Laurent Deogratius Luswetula
Naibu waziri: Mshamu Ali Munde
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Waziri: Balozi Mahmoud Thabit Kombo
Naibu waziri: Dkt. Ngwaru Jumanne Maghembe
Naibu waziri: James Kinyasi Millya
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri: Boniface George Simbachawene
Naibu waziri : Denis Lazaro Londo
Wizara ya Kilimo
Waziri: Daniel Godfrey Chongolo
Naibu Waziri: David Ernest Silinde
Wizara ya Maji
Waziri: Jumaa Hamidu Aweso
Naibu waziri: Kundo Andrea Mathew
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri : Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho
Wizara ya Ujenzi
Waziri: Abdallah Hamis Ulega
Naibu waziri : Mhandisi Godfrey Msongwe Kasekenya
Wizara ya Uchukuzi
Waziri: Prof. Makarne Mbarawa Mnyaa
Naibu waziri : David Mwakiposa Kihenzile
Wizara ya Viwanda na Biashara
Waziri: Judith Salvio Kapinga
Naibu Waziri: Patrobas Paschal Katambi
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Waziri : Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki
Naibu waziri: Switbert Zacharia Mkama
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Mahundi Maalum
Waziri: Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima
Naibu waziri: Maryprisca Winfried Mahundi
Wizara ya Afya
Waziri: Mohamed Omary Mchengerwa
Naibu waziri: Dkt. Florence George Samizi
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Waziri: Prof. Adolf Faustine Mkenda
Naibu waziri: Wanu Hafidh Ameir
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Waziri: Dkt. Leonard Douglas Akwilapo
Naibu waziri: Kaspar Kaspar Mmuya
Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri: Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji
Naibu Waziri : Hamad Hassan Chande
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Waziri: Prof. Palamagamba John Kabudi
Naibu waziri: Hamisi Mwinjuma
Naibu waziri: Paul Christian Makonda
Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Waziri: Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa
Naibu waziri : Ng’wasi Damas Kamani
Wizara ya Madini
Waziri: Anthony Peter Mavunde
Naibu waziri : Dkt. Steven Lemomo Kiruswa
Wizara ya Nishati
Waziri: Deogratius John Ndejembi
Naibu waziri: Salome Wycliffe Makamba
Wizara ya Katiba na Sheria
Waziri: Juma Zuberi Homera
Naibu waziri: Zainabu Athman Katimba