Chris Brown, ameandika ujumbe mfupi kauli ambayo imeonekana kuwa zaidi ya maneno bali ni dira ya maisha.
Kupitia Instagram Stories yake Breezy ameandika “I don’t wanna be rich, I wanna create generational wealth.” Kauli ambayo inaonekana kuelekeza nguvu zake kwenye kujenga msingi imara wa kifedha ambao utawanufaisha sio tu yeye, bali pia watoto wake na vizazi vinavyofuata.
Katika era ambayo wengi wanatafuta utajiri wa haraka, Chris Brown anaonesha mtazamo tofauti, kuwekeza kwenye urithi, sio umaarufu wa leo tu. Inaonyesha jinsi msanii huyo anavyokomaa kimawazo sambamba na mafanikio yake ya muziki.
Kwa upande wa mashabiki wa Team Breezy, ujumbe huu ni kama mwendelezo wa safari yake kutoka kuwa dansa mwenye kipaji, hadi kuwa mmoja wa wasanii wanaoheshimiwa zaidi duniani, sasa akiyatafsri maisha nje ya muziki.