Biilionea Elon Musk amerudi kwenye vichwa vya habari, safari hii sio kuhusu roketi, x wala Tesla, bali kwa jina la Bad Bunny.
Kupitia mahojiano mapya, Musk alitania kuwa hana chochote dhidi ya Bad Bunny lakini akadai jina hilo linawapa watoto ujumbe usiofaa akisisitiza kuwa sungura sio wabaya.
Bilionea huyo alienda mbali zaidi, na akatangaza Dau la dola millioni 67 (takribani bilioni 163, iwapo msaniii huyo atachagua kujiita Good Bunny badala ya Bad Bunny kama anavyofahamika).
Kauli hiyo imeasha maoni mchanganyiko mtandaoni baadhi wanasema ElonMusk anafanya promo ya Super Bowl huku wengine wanaamini ni utamaduni wake wa kuanzisha mijadala bila sababu.
BadBunny bado yupo kimya, na mashabiki wake wana subiri kuona kama atarudisha kombora au kugeuza utani huu kuwa muendelezo wa kutrend kabla ya halftime show.