Jiji la Atlanta, nchini Marekani, limetangaza rasmi Novemba 18 kuwa “Davido Day, siku maalum ya kumuenzi staa wa Afrobeats, Davido.
Heshima hii ilianza kutolewa mwaka 2023 baada ya msanii huyo kuuza tiketi zote kwenye ukumbi wa State Farm Arena wenye uwezo wa kubeba watu 21,000 tukio lililotajwa kama moja ya mafanikio makubwa ya muziki wa Kiafrika nchini Marekani.
Ingawa Davido alizaliwa Novemba 21, Atlanta ndiyo mji alikozaliwa, hivyo jiji hilo limekuwa na uhusiano wa karibu na safari yake. Kupitia “Davido Day,” Atlanta inatambua mchango wake katika kukuza Afrobeats kimataifa, kuunganisha diaspora ya Kiafrika, na kuibua ushawishi mkubwa katika muziki wa kizazi kipya.
Kwa kutangaza siku hii, Atlanta imeweka alama ya heshima kwa msanii ambaye ameigeuza Afrobeats kuwa harakati ya dunia na kuifanya Atlanta kuwa sehemu ya hadithi hiyo ya mafanikio.