Baada ya miezi kadhaa ya kutawala mitandaoni, kuzungumziwa kwenye makundi ya burudani, na kuwa gumzo kwa mashabiki, hatimaye Mama Amina amefanikisha kupata kolabo na “Chino Kidd” hatua ambayo wengi walikuwa wakiisubiria.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Chino Kidd amethibitisha ujio wa kazi hiyo mpya kwa kusema:“MAMA AMINAA IS BACK AGAIN ZIKIFIKA COMMENT 2000 TUU TUNAACHIA LEO LEO 17:00 JIONI.”
Kolabo hii imekuwa ikisubiriwa muda mrefu, hasa baada ya Mama Amina kujijengea jina kama mmoja wa mastaa wapya Tanzania mwenye mvuto wa aina yake na uhalisia unaowavutia mashabiki kila kona.
Hii inaweza kuwa ngoma itakayoitikisa TikTok, kupitia vituko vya Mama Amina na style ya Chino Kidd inayokubalika kwa mashabiki wake.