Mwili wa Mtanzania aliyeuawa Israel, Joshua Mollel umewasili nyumbani kwao Mtaa wa Njiro mji mdogo wa Orkesumet wilayani Simanjiro mkoani Manyara kwa ajili ya maziko.
Mabaki ya mwili wa Joshua yaliwasili nchini jana Novemba 19, na kupokewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Saidi Shaib na Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Fakii Lulandala kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Dada wa marehemu, Hosiana Mollel na msemaji wa familia Efatha Nanyaro wamezungumza wameeleza namna hali ilivyo baada ya kupokea mabaki ya ndugu yao kuwa ni simanzi.
Joshua Mollel alizaliwa Mei 18, mwaka 2002 mji mdogo wa Orkesumet na kuuawa na wapiganaji wa Hamas katika mapigano ya Israel na Palestina ukanda wa Gaza Oktoba 7, 2023.
Kufika kwa Mabaki ya Joshua nyumbani kwako inatajwa kuwa ni faraja na hatima yake hapa duniani kwa kuwa wameuona mwili wake kuliko siku za nyuma walipo kuwa gizani kujua hatima ya kijana wao aliyekuwa Israel kwa masomo ya Kilimo, na Kupoteza mawasilaiano yake toka Oktoba 07-2023 lilipotokea shambulizi La Hamasia na kuuwa zaidi ya watu 1,200.