Muimbaji The Weeknd ameweka historia mpya kwenye muziki wa dunia baada ya ziara yake ya After Hours Til Dawn kuingiza zaidi ya dola bilioni 1, na hivyo kumfanya kuwa msanii wa kiume mwenye ziara iliyowahi kuingiza pesa nyingi zaidi katika historia ya muziki.
Ziara hiyo iliyoanza mwaka 2022 imezunguka mabara mbalimbali, ikijaza viwanja vikubwa na kuvunja rekodi za mahudhurio ya mashabiki, ubunifu wa jukwaa, pamoja na matumizi ya teknolojia ya hali ya juu.
Kwa mara nyingine, The Weeknd amethibitisha kuwa ni miongoni mwa wasanii wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani.
Hii ni hatua kubwa katika tasnia ya muziki na inaweka jina lake kwenye rekodi za milele, akiongoza orodha ya wasanii wa kiume walioingiza mapato makubwa kupitia ziara za muziki.