Mtayarishaji wa muziki Bin Laden (@ladengatz) amefichua hadharani kwamba hajawahi kulipwa hata siku moja kwa kazi alizomfanyia Roma Mkatoliki (@roma_zimbabwe.
Bin Laden ameeleza kuwa baada ya madai yake kuingia kwenye vyombo vya habari, Roma hakuwahi kumtafuta, kumwomba radhi, wala kutoa kauli yoyote kuhusu tuhuma hizo, jambo lililomfanya aamini kuwa Roma alimdharau na hakuwahi kuthamini mchango wake kama producer.
Bin Laden amesema wazi kuwa kitendo cha Roma kutonyoosha jambo hilo, licha ya kujua ukweli, kimemfanya amuite: “Mbinafsi…. Hakutaka nione pesa hata siku moja.
Ameeleza kuwa alifanya kazi nyingi kwa imani na uaminifu, lakini alichokipata ni kudhulumiwa kimfumo, huku kazi zikimpa mafanikio msanii lakini si kwa upande wa uzalishaji.