Baada ya tukio la kumtoa shabiki ukumbini, gumzo jipya limezidi kushika kasi kuhusu idadi ndogo ya watu walionekana kwenye show ya Burna Boy jijini Texas.
Picha na video zilizosambaa mtandaoni zinaonyesha sehemu kubwa za viti zikiwa wazi, hali ambayo imeibua maswali kuhusu nini hasa kilitokea kwenye tamasha hilo.
Ingawa ukumbi una uwezo wa kukusanya zaidi ya watu 18,000, madai yanayozunguka mitandaoni yanasema tiketi zilizouzwa zilikuwa 2,000 tu. Hata hivyo, hakuna taarifa rasmi iliyothibitisha idadi hiyo kutoka kwa waandaaji, jambo linaloacha nafasi ya mjadala na tafsiri nyingi tofauti.
mashabiki wanasema tukio la kumtoa shabiki jukwaani limeongeza uzito wa mjadala, huku wengine wakiona kama ishara kuwa msanii huyo ana uhusiano mgumu na mashabiki wake katika baadhi ya majiji ya Marekani.
Licha ya hayo, Burna Boy bado anabaki kuwa mmoja wa wasanii wa Afrika wenye mafanikio makubwa duniani, na show moja iliyoonekana tupu haiwezi kufuta rekodi zake za kuujaza ukumbi huo mara mbili.