Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amewasihi wananchi kudumisha amani na kushirikiana na Jeshi la Polisi kuimarisha usalama wa Taifa.
Kauli hiyo imekuja Jana Novemba j25 2025 wakati akitembelea baadhi ya vituo vya Polisi vilivyochomwa moto katika vurugu jijini Dar es Salaam wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 2025 ikiwemo Ubungo, Temboni, Mbezi Juu na Salasala.
Waziri Simbachawene ameeleza kuwa uharibifu wa miundombinu ya vituo hivyo umekwamisha utendaji kazi wa baadhi ya vituo, jambo lililosababisha wananchi kushindwa kupata huduma za kawaida za polisi.
Aidha amewakumbusha wananchi kuwa uharibifu wa mali za Serikali ni kupoteza rasilimali muhimu kwa huduma za wananchi, na Serikali imeanza kurejesha miundombinu hiyo ili kudumisha usalama wa wananchi.