Jeshi la Sudan limesema limezuia shambulizi la wanamgambo wa RSF kwenye mji muhimu kusini mwa nchi hiyo jana Novemba 25,2025 huku Marekani ikizihimiza pande zote mbili kukubali pendekezo la kusitisha mapigano.
Jeshi hilo lilizuia shambulizi kwenye kambi yake katika mji wa kimkakati wa Babanusa ambao ni ngome yake kubwa ya mwisho katika eneo hilo.
Babanusa iko kwenye njia muhimu ya usafirishaji kati ya mji mkuu Khartoum kupitia Kordofan na Darfur.
Mjumbe wa Marekani barani Afrika, Massad Boulos akiwa Abu Dhabi jana amesema kuwa pande zote hazijakubaliana na pendekezo jipya la kusistisha mapigano lililoandaliwa na kundi la Marekani, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Misri.