Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ametaka vijana wanaofanya kazi katika sekta ya ujenzi wasifukuzwe kazi kiholela hasa kwa makosa yasiyo ya uaminifu na uzembe.
Waziri Ulega ameyasema hayo katika ziara yake ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa miundombinu inayojengwa chini ya wizara yake jijini Dar wa Salaam.
Ulega amesema amepata malalamiko kutoka kwa baadhi ya vijana wanaodai kuwa wamefukuzwa kazi kwa sababu ya kuwa mstari wa mbele kudai haki za ajira.
Amesema masuala madogo kama ya uonevu kazini matokeo yake hufanya watu kuwa na hasira na Serikali yao kwa mambo ambayo yanazungumzika.
Katika ziara yake hiyo, Ulega ametoa wito kwa wakandarasi ambao hawajakamilisha ujenzi wa barabara kwa mujibu wa wa mikataba kukamilisha haraka kabla Serikali haijavunja mkataba.