Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amekagua ujenzi wa madaraja ya dharura katika Mkoa wa Lindi, na ujenzi huo sasa imevuka asilimia 88.
Madaraja hayo yanajengwa maeneo ya Somanga, Njia Nne na Matandu, sehemu ambazo zimekuwa changamoto wakati wa mvua kutokana na barabara kukatika na kuathiri usafiri kati ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Amesisitiza kuwa wakandarasi wanaendelea kufanya kazi usiku na mchana ili madaraja yote yakamilike ifikapo Desemba 24, 2025, na barabara za maungio na ufungaji wa taa.
Madaraja yaliyokaguliwa ni Somanga Mtama (mita 60) ambalo limefikia asilimia 89, Kipatwa (m 40) asilimia 86.7, Mikereng’ende (m 40) asilimia 90.06 na Njenga/Matandu (m 60) asilimia 86.67.
Waziri Ulega ameeleza kuwa kukamilika kwa madaraja hayo kutamaliza shida za kukatika kwa mawasiliano zilizokuwa zikirudiwa kipindi cha mvua za masika.