BCDEEEE
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchunguzi Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Jaji Mkuu mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Othman Chande amewaomba Watanzania na wadau wengine kuipima tume baada ya kukamilika kwa kazi ya uchunguzi.
Jaji Chande ameyasema hayo wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari leo Desemba 1, 2025.
Jaji Chande ameeleza kuwa wajumbe wa tume hiyo wanaelewa Watanzania wanataka nini, na ameomba wapewe muda ili waweze kuifanya kazi hiyo .
Tume hiyo imeanza rasmi mikutano na wadau, ikitarajiwa kukusanya ushahidi, kupokea maoni ya wananchi, na kufanya uchambuzi wa matukio yote yaliyojiri katika kipindi husika kabla ya kutoa ripoti yake rasmi.
Katika shughuli hiyo Tume inatarajia kufanya Uchunguzi katika mambo ya fuatayo
1.Kuchunguza na kubaini chanzo halisi cha matukio wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi
2.Kuchunguza lengo lililokusudiwa na wale ambao tutaona walikuwa wamepanga na kutekeleza vitendo hivyo yaani lengo lao.
3.Kuchunguza na kubainisha madhara yaliyojitokeza ikiwemo vifo majeruhi uharibifu wa mali na madhara ya kiuchumi na kijamii
4.Kuchunguza mazingira na hatua mbalimbali zilizochukuiliwa na serikali na vyombo vyake na mtu yeyote mwingine.
5. Kupendekeza maeneo yanayohitaji kuimarishwa zaidi ili kuongeza uwajibikaji wa viongoz na raia kwenye kulinda amani ya nchi yetu, utawala bora, haki za binadamu, utawala wa sheria hadi kufikia maridhiano ya kitaifa.
6. Kuchunguza jambo lolote ambalo tume itaona ni muhimu na litaendana na majukumu ya tume