Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, amesema Serikali imewekeza shilingi bilioni 189 kutoka vyanzo vya ndani ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma za Ukimwi nchini, baada ya kupungua kwa ufadhili wa kimataifa.
Dkt Samizi ameeleza hayo leo ikiwa ni siku ya UKIMWI Duniani Kote ambayo hufanyika Desema 1 ya kila mwaka
Akizungumza leo Desemba 1, 2025 Jijini Dar es Salaam, Dkt. Samizi amesema fedha hizo zimeiwezesha Serikali kutoa dawa, vitendanishi na kusafirisha sampuli za maabara kote nchini.
Amesema uwekezaji huo umehakikisha upatikanaji wa dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARVs) kwa asilimia 100, bila mgonjwa kukosa dawa anapofika kituoni.
Aidha Dkt Dkt. Samizi amewataka wananchi kuendelea kufuata huduma katika vituo vya afya, ambako wanapata ushauri na matibabu bila malipo.